Virusi vya korona

Corona information Video on Youtube - swahili (Info Gloria)

Karanteeniohje -pdf
Miongozo kwa kipindi cha karantini na cha utengano

Kuvallinen ohje maskin käyttöön -pdf
Maelekezo kwa matumizi ya barakoa, yaani maski

Maelezo juu ya virusi vya korona kwa wakazi wa Jyväskylä

Zuia maambukizi

 • Nawa mikono yako kwa maji na sabuni angalau kwa muda wa sekunde 20.  Kausha mikono yako kwa karatasi safi. Unaweza pia kutumia kitakasa mikono (käsidesi).
 • Usiguse macho yako, pua au mdomo isipokuwa mara baada ya kunawa mikono. 
 • Ukipiga chafya au kukohoa, funika uso wako na tishu. Tupa tishu kwenye chombo cha takataka. Ikiwa huna tishu, kohoa kwenye mkono wa shati lako, siyo kwenye mkono wako.
 • Acha umbali wa angalau mita 2 kati ya wewe na watu wengine.
 • Usiwakaribishe wageni nyumbani, na usiwatembelee watu wengine.
 • Kaa nyumbani ikiwa wewe ni mgonjwa.
 • Tumia barakoa (maski), ikiwa huwezi kuacha umbali wa kutosha kati ya wewe na watu wengine, kwa mfano kwenye usafiri wa umma au wakati wa kwenda kwenye kipimo cha virusi vya korona.

Dalili za korona

Dalili za ugonjwa unaosababishwa na virusi vya korona /(COVID-19) ni kwa mfano homa, kikohozi, shida ya kupumua, uchovu, hali ya kusikia kichefuchefu, harisho, shida kwenye hisia ya ladha au ya harufu.

Ugonjwa huu unaweza kuwa ni wa hatari hasa kwa wazee na kwa wale wenye magonjwa mengine, kwa mfano magonjwa ya mapafu na ya moyo.

Wasiliana na maulizo ya korona, ikiwa unasikia dalili fulani.

Ikiwa unasikia dalili hata ndogondogo, piga simu kwa nambari ya huduma ya korona ya shirika la afya

 • kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa saa 8 - 16 (kuanzia saa mbili hadi saa kumi); Jumamosi na Jumapili saa 9 - 15 (kuanzia saa tatu hadi saa tisa). Nambari ni 014 266 0133.    
 • Wakati mwingine piga simu kwa nambari ya dharura, 116 117. 
 • Ukihitaji kuwa na mkalimani eleza ombi hili kwenye simu.   
 • Wale wenye shida ya kutokusikia wanapewa muda kwa kipimo na matokeo yake kwa kupitia ujumbe wa simu kwenye nambari ya 050 303 7722.

Unaweza kujibu maswali kuhusu dalili zako kwenye mtandao. Tafuta huduma inayoitwa Omaolo (kwa Kifini, Kiswedi au Kiingereza). Ikiwa mwenye dalili ni mtoto, piga simu kwa nambari ya korona ya shirika la afya, 014 266 0133. Kwa kupitia huduma ya Omaolo (makisio ya dalili) kwenye mtandao unaweza pia kupanga muda kwa kipimo cha virusi vya korona.

Wafanyakazi wa shirika la afya kwenye simu wanakadiria umuhimu wa kupimwa kwako. Kwenye simu unapewa maelezo yafuatayo: ufanye nini, uende lini kwa kipimo na uende wapi kwa kupimwa.

Matokeo ya kipimo cha virusi vya korona yanatumwa kwa njia ya ujumbe wa simu.

Ikiwa umeenda kupimwa, kaa nyumbani muda wote kuanzia siku ya kupimwa hadi siku ya kupata matokeo.  Epuka kuonana na watu nje ya familia yako. 

Ikiwa matokeo ya kipimo cha virusi vya korona yanaonyesha kwamba (negatiivinen) huna ugonjwa wa korona, isipokuwa ni mafua ya kawaida tu, pumzika nyumbani ili usiwaambukize wengine. 

Ikiwa matokeo ya kipimo chako cha virusi vya korona (COVID-19) yanaonyesha kwamba (positiivinen) umepata ugonjwa huu wa korona, subiri nyumbani mpaka nesi akupigie simu. Fuata miongozo unayoipewa na nesi.

Ikiwa wewe ni mgonjwa, usiende dukani.

Ikiwa wewe ni mgonjwa, usiende dukani wala kwenye duka la madawa. Omba msaada kutoka kwa ndugu au majirani. Maduka ya chakula na maduka ya madawa yanatoa huduma ya kuleta manunuzi mpaka nyumbani. Ukishindwa kupata msaada, omba msaada kutoka katika mji wa Jyväskylä. 

 • Wakazi wa Jyväskylä: kuanzia Jumatatu hadi Jumatano saa 9 - 14 (kuanzia saa tatu hadi saa nane) nambari 014 266 0550. 
 • Wakazi wa Hankasalmi: kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa saa 8 - 16 (kuanzia saa mbili hadi saa kumi), nambari 014 267 1490.
 • Wakazi wa Uurainen: kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa saa 8 - 16 (kuanzia saa tatu hadi saa kumi), nambari 040 772 8543

Wakati mwingine wakazi wa Jyväskylä, Hankasalmi na Uurainen wanapewa msaada pia kwa kupitia huduma ya dharura ya usitawi wa jamii, nambari 014 266 0149. 

Tumia barakoa ya uso.

Wakazi wa Jyväskylä zaidi ya umri wa miaka 12 wamepewa pendekezo la kutumia barakoa ya uso. 

Tumia barakoa ikiwa huwezi kuwa na umbali wa kutosha na watu wengine, kwa mfano 

 • ndani ya majengo ya hadhara, madukani, maktabani, kwenye vituo vya vijana, makanisani, kwenye jumba la maonyesho (teatteri) au kwenye ukumbi wa muziki (konserttisali)
 • kwenye mikutano ya watu wengi, kwenye michezo inayofanyika nje na kwenye matukio ya msongamano
 • kwenye shule za sekondari na vyuo mbalimbali 
 • kwenye usafiri wa umma
 • kwenye safari ya kwenda kwenye kipimo cha virusi vya korona
 • ukifika Finland kutoka eneo la hatari la korona

Usitumie barakoa, ikiwa inaleta shida kubwa kwa kupumua kwako au ikiwa wewe una sababu nyingine za afya zinazokuletea shida ukitumia barakoa.

Vituo vya ugawaji wa barakoa

Mji wa Jyväskylä unagawa barakoa kwa wakazi wake maskini  Kwa kawaida wakazi wanajinunulia wenyewe barakoa.zao Watu zaidi ya umri wa miaka 12 wanapendekezwa kutumia barakoa.

Barakoa zinagawiwa kwenye vituo vifuatavyo:

 • Kituo cha huduma ya usitawi wa jamii Hannikaisenkatu (Hannikaisenkadun sosiaaliasema), Hannikaisenkatu 37; kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa saa 10 - 14 (kuanzia saa nne hadi saa nane).
 • Ofisi ya huduma ya kuwazoeza wahamiaji wapya (Kotoutumispalvelut), Väinönkatu 1; kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa saa 10.00 - 13.00 (kuanzia saa nne hadi saa saba)
 • Vituo vya afya:
  • Mjini kati (Keskusta), Kuokkala, Kyllö, Palokka na Sampoharju, Jumanne na Alhamisi, saa 12 - 16 (kuanzia saa sita hadi saa kumi)
  • Korpilahti, Säynätsalo na Tikkakoski, Jumanne na Alhamisi, saa 14 - 16 (kuanzia saa nane hadi saa kumi)
 • Ofisi ya kijiji ya Huhtasuo (Huhtasuon kylätoimisto), Nevakatu 1, Jumatatu hadi Alhamisi saa 9 - 15 (saa tatu hadi saa tisa) na Ijumaa saa 9 - 14 (kuanzia saa tatu hadi saa nane)
 • Ukumbi wa Matara/Gloria (kituo cha shughuli za kiraia), Matarankatu 6 A, kuanzia Jumatatu hadi Alhamisi saa 9 - 16 (kuanzia saa tatu hadi saa kumi), Ijumaa saa 9 - 14 (kuanzia saa tatu hadi saa nane).

Ikiwa umewekwa kwenye karantini au utengano  

Omba kutoka kwa nesi wako miongozo (kwenye lugha yako) juu ya karantini. Ni muhimu kufuata miongozo. Miongozo ya ziada inapatikana kutoka katika wavuti za karantini https://www.jyvaskyla.fi/terveys/korona/karanteeni  

Pakua programu ya kihisio cha korona (koronavilkku) kwenye simu yako 

Ni programu inayokuarifu ikihisi kwamba umekuwa karibu na mtu ambaye ana ugonjwa wa korona Kihisio cha korona kinaweza kupakuliwa bila malipo kutoka  https://koronavilkku.fi/

Taarifa zaidi:

Wavuti za korona za mji wa Jyväskylä: https://www.jyvaskyla.fi/terveys/korona  

Information on the Coronavirus in Jyväskylä in English
https://www.jyvaskyla.fi/en/health-care-and-social-services/healthcare-services/information-coronavirus-jyvaskyla

Taarifa juu ya virusi vya korona mjini Jyväskylä - lugha nyingine  / Information on the Coronavirus in Jyväskylä – other languages https://www.jyvaskyla.fi/terveys/korona/muutkielet 

Taarifa ya kisasa kutoka wavuti kwa Kiingereza: Finnish Institute of Health and Welfare (Taasisi ya afya ya usitawi ya FInland, Terveyden ja hyvinvoinnin laitos THL): https://thl.fi/en/web/infectious-diseases-and-vaccinations/what-s-new/coronavirus-covid-19-latest-updates

Maelezo juu ya maamuzi ya serikali ya Finland kuhusu virusi vya korona kwa Kiingereza: https://valtioneuvosto.fi/en/information-on-coronavirus